Kombe la Dunia: Ghana yaipa matumaini ya ushindi Afrika

  • | VOA Swahili
    367 views
    Mwaka 2010 Ghana ilikuwa timu ya tatu barani Afrika kufikia robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia huku ikibeba matumaini ya bara hilo huko Afrika Kusini. Walimaliza mbele ya Australia na Serbia, katika kundi lao kisha wakawashinda Wamarekani kabla ya kushindwa kwa mikwaju ya penalti baada ya utata katika mechi dhidi ya Uruguay mjini Johannesburg. Baada ya kushiriki vibaya nchini Brazil miaka minne baadae Ghana wamerejea katika hatua kubwa ya soka duniani. Sikiliza uchambuzi wa mwandishi wa VOA akiwa nchini Qatar... #voaworldcup2022 #fifaworldcup #worldcup #qatar #qatar2022 #fifa #football #messi #soccer #ronaldo #futbol #futebol - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.