- 8,162 viewsDuration: 44sVideo kutoka kituo cha televisheni cha Urusi, RT, imenasa tukio ambapo kombora lilitua umbali wa mita chache tu kutoka mahali mwandishi wa kituo hicho alikuwa anaripoti moja kwa moja kusini mwa Lebanon RT ilisema kuwa Steve Sweeney pamoja na mpiga picha wake wanapatiwa matibabu hospitalini. BBC imethibitisha video hiyo kuwa ni ya kweli. Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga na operesheni za ardhini kusini mwa Lebanon dhidi ya kundi la wanamgambo la Hezbollah. #bbcswahili #lebanon #RT Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw