Korti yadinda kusitisha mpango wa Lishe Shuleni katika kaunti Nairobi

  • | Citizen TV
    755 views

    Mahakamama kuu imekataa kusimamisha mpango wa Lishe shuleni ulioanzishwa na kaunti ya Nairobi hivi majuzi. Jaji Mugure Thande akitoa uamuzi wake amesema kuwa kusimamisha mradi huo kutakuwa ni kuwadhulumu watoto wanaotegemea kupata chakula shuleni. Mawakili Duncan Okatch na Elius Mutuma wakitoa hoja zao waliambia mahakama kuwa mradi huo ni wa manufaa kwa wanafunzi ambao wanatozwa shillingi tano kila siku na ni afueni kwa wazazi wanaogharamika tu shilingi elfu moja kwa mwaka.