Korti yaruhusu mshukiwa anayedaiwa kufyatua risasi iliyomuua Charles Were kuzuiliwa kwa siku 30

  • | Citizen TV
    5,154 views

    Mshukiwa anayeaminika ndiye aliyefyatua risasi iliyomuua mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were amefikishwa mahakamani. Isaac Kuria ataendelea kuzuiliwa kwa siku 30 huku uchunguzi wa mauwaji ya mbunge huyo ukishika kasi. Uchunguzi wa awali umemhusisha Kuria moja kwa moja na bunduki iliyotumika kumuuwa mbunge huyo pamoja na mawasiliano kati yake na washukiwa ambao tayari wako korokoroni.