KRA yajitenga na sakata ya sukari haramu nchini

  • | Citizen TV
    1,792 views

    Halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini KRA sasa inajitenga na sakata ya sukari iliyoharamishwa ikijiondolea lawama ya makosa yoyote. KRA sasa ikisema haikuwa na jukumu lolote lililosababisha kuachiliwa kwa sukari hiyo kuuzwa sokoni. Kwenye ripoti ya bunge la bunge la kitaifa inayochunguza sakati ya sukari hiyo, KRA imesema kwamba jukumu lake lilikuwa tu kuhusiana na ushuru.