- 16,149 viewsDuration: 1:05Tazama jinsi baba huyu alivyoshindwa kujizuia machozi ya furaha mwanawe aliporudi nyumbani baada ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na Ukraine. Alieleza kuwa kijana wake ni fundi ujenzi na mekaniki stadi na sasa amerudi salama. Kubadilishana huku nadra kulitokea baada ya siku mbili za mazungumzo ya amani yaliyoratibiwa na Marekani huko Abu Dhabi. Jumla ya Waukraine 157 wakiwemo raia saba na wanajeshi 157 wa Urusi walirejea nyumbani. Ni mabadilishano ya kwanza ya aina hii ndani ya miezi minne. - - #bbcswahili #ukraine🇺🇦 #urusi #wafungwa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw