Kundi jipya la damu lenye mtu mmoja

  • | BBC Swahili
    6,594 views
    Katika ulimwengu wa tiba, kumegunduliwa kwa kundi jipya kabisa la damu lijulikanalo kama Guadeloupe Negative kumewashangaza wataalamu wa afya duniani. Hadi sasa, mtu mmoja tu anafahamika kuwa na damu hii ya kipekee isiyo na antijeni ya EMM, jambo linalomaanisha hawezi kuongezewa damu kutoka kwa mtu mwingine yeyote duniani. Ugunduzi huu si wa kubahatisha, bali ni ushahidi wa ajabu wa jinsi mwili wa binadamu unavyobeba siri kubwa zisizoisha. Mwandishi wa BBC @frankmavura ameiangazia habari hii kwa kina Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw