Kundi la G7 laanza kuibana Russia isitumie mafuta kufadhili vita vyake Ukraine

  • | VOA Swahili
    158 views
    Kundi la nchi saba tajiri maarufu kama G7 limeweka bei ya mafuta ghafi ya Russia hatua hiyo imeanza Jumatatu (Desemba 5) wakati nchi za Magharibi zikijaribu kuibana Moscow isiwe na uwezo wa kufadhili vita yake nchini Ukraine, lakini Russia imesema haitaheshimu hatua hiyo hata kama itamaanisha kupunguza uzalishaji wa mafuta. Bei iliyowekwa, ambayo itatekelezwa na kundi la G7, Umoja wa Ulaya na Australia, inakuja kuongezea shinikizo lililoko la vikwazo vya EU kwa bidhaa zinazoingizwa za mafuta. - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.