Kundi la waislamu la kwenda kuhiji latapeliwa maelfu ya pesa

  • | Citizen TV
    3,425 views

    Kundi la waislamu kutoka maeneo mbalimbali nchini linalilia haki baada ya kutapeliwa maelfu ya pesa kwenye mpango wa kugharamia safari ya Hajj na Umrah katika mji mtakatifu wa makkah. Waathiriwa wanadai kuwa Imamu Ustadh Omar Athman, wa msikiti wa Ihsan mjini Malindi kaunti ya Kilifi, aliwaahidi kuwapeleka kuhiji lakini ahadi hiyo ikawa ndoto baada ya mtuhumiwa kutoweka na pesa zao.