KUPPET yasema wazazi watalipa karo kufidia ukosefu wa fedha shuleni

  • | Citizen TV
    391 views

    Muungano wa Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET) umetangaza kuwa wazazi watalazimika kulipa karo kuanzia muhula ujao. Hali hii imesababishwa na kucheleweshwa mara kwa mara kwa mgao wa fedha zinazohitajika ili kufanikisha shughuli za masomo katika shule za umma nchini. Shule nyingi nchini zimejipata kwenye njia panda kutokana na ukosefu wa afedha za kuendesha shughuli, kiasi cha kukatiza kalenda ya masomo ya muhula huu na kutishia kufunga shule mapema.