‘Kuwa makini na mtu anayesema anataka kujiua’ - Mwanasaikolojia

  • | BBC Swahili
    586 views
    Shirika la Afya Duniani WHO linasema mtu 1 katika kila watu 8 duniani ana matatizo ya afya ya akili. Nchini Tanzania, watu 5 kati ya 100,000 hujiua kutokana na matatizo ya afya ya akili kama vile wasiwasi, huzuni, hasira na matumizi ya dawa za kulevya katika miaka mitano iliyopita. Kijana mmoja kutoka Tanzania ameanzisha shirika linalowakutanisha vijana ili kujadili mada mbalimbali ikiwemo namna wanavyoweza kupambana na matatizo ya afya ya akili. Mwandishi wa BBC @elizabethkazibure ametuandalia taarifa hii 🎥: @frankmavura #bbcswahili #tanzania #who