Kwa nini Marekani inataka kuwapeleka wahamiaji Rwanda?

  • | BBC Swahili
    301 views
    Serikali ya Rwanda imesema nchi hiyo itawapa hifadhi wahamiaji waliofurushwa kutoka Marekani. Kwa mujibu wa msemaji wa Rwanda, Yolande Makolo, wahamiaji 250 huenda wakaingia Rwanda chini ya makubaliano hayo. Wale walioidhinishwa na maafisa wa serikali ya Rwanda watapewa mafunzo ya kikazi na watapokea huduma za afya. Na pia watapewa makazi watakapoingia nchini humo.