- 155 viewsDuration: 10:27Wizara ya elimu nchini Kenya imesema kwamba haitalazimika kutoa amri ya kufunga shule mapema ili kuzuia ghasia zaidi katika shule za upili muhula huu, ikiahidi kuweka mikakati zaidi kuhakikishia wanafunzi usalama. Wiki iliyopita, wanafunzi 16 waliuawa kutokana na moto kwenye bweni katika shule ya upili ya wasichana ya Utumishi. Wanafunzi tisa wanashikiliwa kuhusiana na kisa hicho. Lakini hii sio mara ya kwanza kwa visa kama hivi kutokea. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasema limekabiliana na visa 37 vya moto katika shule tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Hii imeibua maswali mengi - je, ni nani wa kulaumiwa na tatizo hasa liko wapi? Ili kufahamu zaidi, Roncliffe Odit amezungumza na mwanasaikolojia Serah Wanjiru, pamoja na Boaz Waruku, mshauri wa sera katika shirika la Elimu Bora. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw