Lori lililoabiriwa na vijana lasombwa na mafuriko ya mto Muswii

  • | K24 Video
    711 views

    Shirika la msalaba mwekundu limeopoa miili mitano na kuokoa watu 11 waliokuwa miongoni mwa vijana walioabiri lori lililosombwa na mafuriko ya mto muswii eneo la sultan kaunti ya Makueni. Inaarifiwa ajali hiyo ilitokea wakati vijana wasiojulikana idadi ambao walikuwa wameshindwa kuvuka mto uliofurika kuabiri lori hilo dereva alipoamua kuvuka mto huo. Hayo yanajiri huku maafa zaidi yakiripotiwa katika maeneo mbali mbali nchini.