LSK yataka serikali kuwafidia wakulima walioathirika na mbolea feki

  • | Citizen TV
    220 views

    Chama cha mawakili nchini sasa kimeipa serikali siku saba kuwafidia wakulima walioathirika na mbolea bandia la sivyo wawasilishe kesi mahakamani. Kwenye kikao na wanahabari, chama cha LSK kinasema kesi hiyo itawasilishwa kwa pamoja mahakamani, huku kikiwataka wakulima walioathirika kuandikisha malalamishi yao kwenye ofisi za lsk kote nchini. Rais wa lsk faith odhiambo akimtaka waziri wa kilimo, maafisa wakuu wa bodi ya NCPB na wale wa KEBS kuwajibikia sakata hii.