Luhaga Mpina wa ACT Wazalendo azimwa na Msajili wa Vyama, Tanzania

  • | BBC Swahili
    1,689 views
    Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania imebatilisha uteuzi wa mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, ikidai kwamba uteuzi wa mgombea huyo haukufuata taratibu za chama. Uamuzi huu wa Msajili unafuatia malalamiko yaliyotolewa na Katibu Mwenezi wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam Monalisa Ndala aliyedai chama chake kilivunja kanuni katika kumteua Mpina kuwa mgombea.