Maafisa 2 wakuu wa polisi wafikishwa kortini Nyahururu kwa hatia ya ufisadi

  • | Citizen TV
    Maafisa wawili wakuu wa polisi wamefikishwa mahakamani mjini Nyahururu ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi. Maafisa hao wawili Jane Kavutha na Ephraim Karani walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Judith Wanjala ambapo walikana mashtaka hayo. Wawili hao walikamatwa wiki jana mjini Nyeri katika afisi za tume ya ufisadi EACC. Inasemekana wawili hao waliitisha hongo ya zaidi ya shilingi laki nane kutoka kwa wakaazi wa Nyeri mnamo mwaka 2018 walipokuwa wanafanya kazi katika eneo hilo. Waliachiliwa kwa dhamana pesa taslimu shilingi laki mbili. Kesi hiyo itatajwa tena mnamo Machi 23.