Maafisa 3 mahakamani Kenya kufuatia ufichuzi wa BBC Africa Eye wa biashara ya wizi wa watoto

  • | BBC Swahili
    Tuliyonayo katika Dira ya Dunia , Jumatano 18th Nov 2020 • Polisi nchini Kenya wawakamata watu watatu kufuatia uchunguzi uliofanywa na BBC Africa Eye uliofichua biashara inayohusisha wizi wa watoto jijini Nairobi. • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yatangaza kuumaliza kabisa ugonjwa wa Ebola uliozuka hivi karibuni kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. • Rais Donald Trump amemfuta kazi afisa mkuu wa usalama wa mtandao aliyechapisha nyenzo kupuuzilia mbali madai ya udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa urais uliokamilika. • Mgombea urais kupitia chama cha upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine akamatwa. Ungana na Roncliffe Odit pamoja na Regina Mziwanda kuanzia saa kumi na mbili unusu jioni #DIRAYADUNIA #BBCAFRICAEYE #BobiWine