Maafisa-4 wa polisi washtakiwa kwa mauaji ya mtoto Samantha Pendo

  • | KBC Video
    2,624 views

    Maafisa wanne wa polisi wa ngazi za juu, wameshtakiwa kwa mauaji ya mtoto wa miezi 6 Samantha Pendo katika Kaunti ya Kisumu mnamo mwaka wa 2017. Mkurugenzi wa mashtaka ya umma, aliidhinisha mashtaka mbalimbali dhidi yao ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na mateso. Hata hivyo, maafisa wengine saba wa polisi hawakujumuishwa kwenye hati ya mashtaka. Na kama mwanahabari wetu Ruth Wamboi anavyoripoti, huduma ya kitaifa ya polisi imeifahamisha mahakama kwamba mshukiwa wa kumi na moja Mohammed Baa, ambaye ni afisa wa polisi aliyestaafu bado yuko huru, huku juhudi za kumpata nyumbani kwake huko Wajir zikikosa kuzaa matunda.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive