Maafisa 6 wa KWS wafikishwa Mahakamani Nakuru

  • | Citizen TV
    464 views

    Maafisa sita wa shirika la huduma kwa wanyama pori katika mbuga ya Nakuru wamefikishwa Mahakamani Nakuru kufatia kupotea Kwa mvuvi mmoja katika mbuga hiyo. Brian Odiambo aliripotiwa kutoweka tarehe kumi na nane mwezi Februari mwaka huu mikononi mwa maafisa hao baada ya kukamatwa alipokua akiingia katika mbuga hiyo Kwa shughuli za uvuvi. kutoweka kwake kukichochea maandamano ya siku kadhaa mjini humo.