- 850 viewsDuration: 2:16Maafisa tabibu nchini wamepinga hatua ya serikali kutaka kusitisha masomo ya matabibu katika kiwango cha shahada wakisema itaathiri utendakazi na utoaji huduma hospitalini. Wakiongea huko Mombasa baada ya kukamilika kwa kongamano la maafisa tabibu nchini wametaka wizara ya afya kutokubali hoja hiyo. Kupitia baraza la chama hicho maafisa hao wanamtaka waziri wa afya aden duale kuchapisha majina ya baraza la bodi ya matabibu wakisema kwa miezi mitano utendakazi wa bodi umeathiri utoaji huduma licha ya rais william ruto kumteua mwenyekiti wa baraza hilo.