Maafisa wa afya wanachunguza tani 1,000 za sukari iliyokuwa miongoni mwa shehena iliyoharibika

  • | Citizen TV
    671 views

    Maafisa wa afya serikali kuu wameanzisha uchunguzi kuhusu shehena ya zaidi ya tani elfu moja za sukari zilizonaswa na halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini KRA kaunti ya mombasa. Kulingana na wakuu wa kampuni ya Mitchell Cotts Freight Kenya Ltd, maafisa wa afya tayari wamechukuwa sampuli kwenye shehena hiyo ili kutoa mwelekeo kuhusu bidhaa hiyo. Mkurugenzi wa mipango katika kampuni hio James Rarieya pia alipuuzilia mbali madai kwamba sukari hiyo tayari imepenya na kuingia katika maduka ya umma nchini. Kati ya makasha 46 ya sukari iliyoagizwa nchini kutoka Mauritius, 13 yanadaiwa kuharibika baada ya meli hiyo kuingia maji.