Maafisa wa DCI wanasa magunia 560 ya mbolea ghushi eneo la Molo

  • | Citizen TV
    617 views

    Maafisa wa upelelezi katika eneo la Molo kaunti ya Nakuru wamenasa magunia 560 ya mbolea inayoshukiwa kuwa ghushi iliyokuwa imepangwa kusambazwa kwa wakulima katika eneo hilo. Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Molo, Timon Odingo amethibitisha kuwa shehena hiyo yenye thamani ya takriban shilingi Milioni 1.4 iliwasilishwa kwa bohari la Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao ya Molo licha ya kukataliwa na Katibu wa wizara ya Kilimo Paul Ronoh kwa msingi kuwa haikuwa imefikia kiwango cha ubora unaohitajika.