Maafisa wa DCI wapata mshipi na bangili zinazoaminika kuwa za mfanyibiashara aliyeuawa Machakos

  • | Citizen TV
    1,978 views

    Maafisa wa upelelezi wamepata mshipi na bangili alichokuwa amevalia mfanyibiashara Jayesh Kumar siku kabla ya kuuawa katika eneo la Kilili, Lukenya kaunti ya Machakos. Vitu hivyo vilipatikana karibu na eneo ambako Kumar aliuawa. Maafisa wa upelelezi walirejea katika eneo hilo kutafuta mabaki ya mwili wake ambao unaaminika kuliwa na wanyama wa porini baada ya kuuawa.