Maafisa wa KMPDU wadai serikali haina nia njema nao

  • | Citizen TV
    175 views

    Chama cha madaktari nchini sasa kinaishutumu serikali kwa kuwa na msimamo mkali kuhusiana na swala la mishahara na kutumwa kwa madaktari wanafunzi. Katibu Mkuu wa KMPDU Daktari Davji Atella kwenye kikao na wanahabari amesema kuwa, licha ya madaktari kuonyesha ari ya kusitisha mgomo wao, serikali kwa upande wake haiko tayari kukubali yale machache wanayotaka. Sasa madaktari hawa wanasisitiza kuwa hawatalegeza msimamo wao kuhusiana na mgomo wa madaktari ulioendelea kwa siku ya 39 hii leo.