Maafisa wa polisi washika doria mpakani Transmara-Kuria

  • | Citizen TV
    571 views

    Maafisa wa usalama wanaendelea kushika doria katika mpaka wa Kuria na Transmara kufuatia uhasama wa mpaka ambao umekuwa ukidorora kwa siku za hivi karibuni. Akizungumza na runinga ya Citizen kwa njia ya Simu, OCPD wa Transmara Kusini Charles Opondo amethibitisha uwepo wa maafisa kutoka vitengo mbalimbali eneo hilo. Wito pia umetolewa kwa wakazi kutoka pande zote mbili kupiga ripoti kwa idara ya usalama kuhusu uvamizi wa aina yoyote eneo la Angata Barrikoi na Gwetembe.