Maafisa wa usalama wanapokea mafunzo Eldoret

  • | Citizen TV
    852 views

    Serikali imezindua taasisi ya kwanza ya kibinafsi ya mafunzo ya maafisa wa usalama mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, katibu katika wizara ya usalama daktari Raymond Omollo alisema kuwa mahafali wataongeza idadi ya maafisa wa usalama kwa manufaa ya kulinda taifa. Kadhalika , serikali imebuni mtaala kwa taasisi za kibinafsi utakaoambatana na mafunzo ya vyuo vya maafisa wa usalama vya serikali.