- 254 viewsDuration: 2:45Aliyekuwa mama wa taifa mama Ngina Kenyatta ametunukiwa tuzo ya heshima kwa jukumu lake la kupigania ujumuishwaji wa wanawake katika huduma za usalama za Kenya. Alitambuliwa katika sherehe za mwaka huu za staara ya wazee zilizofanyika katika uwanja wa Ulinzi complex jijini Nairobi. Hafla hiyo iliandaliwa na shirika la Ushiriki Wema, mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ulioanzishwa na Tessie Musalia, mke wa mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.