Maafisa wakuu kwenye kaunti watakiwa kuwa waadilifu

  • | KBC Video
    Bodi za utumishi wa umma kwenye kaunti pamoja na kamati za mamlaka na haki kwenye mabunge hayo zimetakiwa kuwa msitari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi magatuzini. Kamishna wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi-EACC, Rose Mghoi ambaye alifungua warsha ya siku tatu ya kujenga nyenzo huko Mombasa, aliwahimiza wanachama wa kamati hizo kudumisha maadili wanapotekeleza majukumu yao. Kamishna Mghoi alisema kamati hizo mbili zinapasa kushirikiana katika kupambana na ufisadi na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive