Maandaliza ya CHAN

  • | Citizen TV
    688 views

    Ukanda wa Afrika Mashariki umetunukiwa fursa ya kuandaa Dimba kubwa la soka barani Africa. Kenya, Uganda, na Tanzania zinajiandaa kuwa wenyeji wa pamoja wa kipute cha CHAN Mwezi Februari 2025 na AFCON 2027. Licha ya Rais wa CAF, Patrice Motsepe, kutoa hakikisho kwamba mchuano wa CHAN utafanyika kama ilivyoratibiwa, Kenya iko chini ya shinikizo la kuboresha viwanja vyake vya Nyayo na Kasarani kabla ya maandalizi. Kwa upande mwingine, Tanzania imeafikia vigezo vya CAF, huku nyanja za Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na Amaan mjini Zanzibar vikiwa tayari kwa ngarambe hiyo. Uganda pia ikijizitati kwa kuandaa Uwanja wa Kimataifa wa Mandela, Namboole.