Maandamano Kenya: Wawili waripotiwa kuuawa

  • | BBC Swahili
    12,427 views
    Watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya polisi kufyatua risasi wakati wa maandamano nchini Kenya, kufuatia makabiliano baina ya waandamanaji na polisi katika maeneo mengi ya mji wa Nairobi, na katika sehemu zingine za nchi. Mamia ya abiria walioingia jijini Nairobi pia wamelazimika kusalia kwenye magari baada ya barabara kuu zinazoingia jijini humo kufungwa. Maandamano haya yanafanyika katika siku ya Saba Saba (tarehe 7 Julai), siku inayotumika kama ukumbusho wa kujitolea kwa Wakenya katika mapambano ya demokrasia ya vyama vingi. Haya yote yanamaanisha nini kwa mustakabali wa taifa la Kenya? @RoncliffeOdit anatuletea hayo na mengine mengi katika Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wa YouTube BBC Swahili.