Maandamano yameenea katika miji 80 nchini Iran

  • | BBC Swahili
    701 views
    Machafuko nchini Iran yameenea katika miji zaidi ya 80, huku watu kadhaa wakiwa wameuawa, kwa mujibu wa mashahidi na mashirika ya kutetea haki za binadamu. Miongoni mwa walioripotiwa kuuawa ni mvulana wa miaka 16. Ghasia hizo zimeanza baada ya kifo cha Mahsa Amini - msichana aliyekamatwa na polisi wa maadili kwa kosa la kuvaa hijabu yake kinyume na masharti ya nchi hiyo. #bbcswahili #uislamu #hijabu #iran