Mabalozi 12 wa kigeni nchini waunga vijana kuandamana

  • | Citizen TV
    1,861 views

    Mabalozi 12 wa kigeni nchini wametaka uhuru wa vijana kuandamana kuzingatiwa huku wakionya dhidi ya utumizi wa wahuni kwenye maandamano yaliyopangwa hapo kesho. Mabalozi hawa wa Marekani, Uingereza na Ujerumani wametaka serikali kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani. Wakati huo huo, Viongozi wa kanisa katoliki nchini pia wametaka uwajibikaji wa polisi wakati wa maandamano hayo huku wakiwataka vijana kuzingatia uwajibikaji na amani