- 190 viewsDuration: 2:26Muungano wa Madaktari KMPDU umetoa makataa ya mgomo kwa Serikali ya Kaunti ya Meru, wakiitaka kutatua malalamishi ya madaktari Meru kabla ya tarehe 6 mwezi ujao la sivyo Madaktari wote wa kaunti hiyo watasusia kazi. Muungano huo umeshutumu utawala wa kaunti kwa kuwawekea madaktari masharti duni ya kimkataba, kucheleweshwa kupandishwa vyeo, na fursa finyu za kujiendeleza kikazi.