Madaktari kuanza mgomo wa kitaifa saa sita leo usiku

  • | Citizen TV
    466 views

    Huenda huduma za matibabu zikatatizwa kuanzia hapo kesho, pale madaktari watakapoanza mgomo wao wa kitaifa. Hii ni baada ya chama cha madaktari nchini kmpdu kutangaza kuanza kwa mgomo huo kuanzia saa sita usiku wa leo. Katibu mkuu wa KMPDU Dkt. Davji atellah amesema serikali haijaonyesha nia ya kushughulikia malalamishi yao, na imeshindwa kuheshimu mkataba wa maelewano wa mwaka 2017.