Madaktari waliogoma katika kaunti ya Kiambu hawatapokea mishahara yao hadi warejee kazini

  • | K24 Video
    82 views

    Madaktari waliogoma katika kaunti ya Kiambu hawatapokea mishahara yao hadi warejee kazini, Ni tangazo lilitolewa na gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi, huku akiongeza kuwa watakaokataa kurejea kazini watachukuliwa hatua za kinidhamu, naye waziri wa leba Florence Bore​​​​​​ amewarai madaktari waliogoma wasikaidi maagizo ya korti na badala yake warejee kazini na kufanya mazungumzo. Huku mgomo ukitimiza mwezi mmoja sasa, seneta maalum wa UDA Miraj Abdilah amemtetea waziri wa afya Susan Nakhumicha akidai mkataba wa CBA wa mwaka wa 2017 ulitumika kisiasa na serikali iliyopita bila mpango wa kuutekeleza.