Madaktari wasisitiza maandamano yataendelea jijini Nairobi

  • | Citizen TV
    1,041 views

    Misimamo mikali kati ya wafanyakazi wa huduma ya afya na baraza la magavana inaendelea kushuhudiwa, baada ya baraza hilo kutangaza kuwa halitatekeleza makubaliano ya pamoja ya 2017 kwani yatakuwa na athari kwa wafanyakazi wengine wa kaunti. Haya yanajiri huku madaktari wakiapa kuendelea na mgomo wao hadi pale makubaliano hayo yatatekelezwa.