Madaktari watishia kugoma iwapo hawataongezewa mishahara

  • | Citizen TV
    411 views

    Muungano wa Madaktari nchini KMPDU umetishia kufanya mgomo wakidai nyongeza ya mishahara. Katibu Mkuu wa muungano huo, Davji Bhimji anasema swala la mishahara ya madaktari halijashughulikiwa kwa miaka 7 iliyopita licha ya kuwa gharama ya maisha imepanda. Aidha ameelezea kuwa baadhi ya kaunti zimewaachisha kazi kiholela madaktari na kwamba mgomo utafanyika iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.