Madereva wa teksi Mombasa watakiwa kufuata sheria

  • | Citizen TV
    330 views

    Naibu kamishna wa kaunti eneo la Nyali amewataka madereva wa texi za mitandao kuzingatia sheria wakati wanapotoa huduma hiyo hasa usiku. Wakizungumza katika warsha iliowaleta pamoja na halmashauri ya usalama barabarani NTSA, maafisa wa polisi pamoja pamoja na wadau katika sekta ya uchukuzi wamedai kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakiwabeba wateja wakiwa walevi au kutumia miraa. Aidha wadau katika sekta ya mtandao kutoka yego wametaka ushirikiano kati ya serikali na wanaotoa huduma hiyo ili kuhakikisha Mombasa ambayo inanawiri kupitia utalii imenufaika na kuboreka kwa utoaji huduma za uchukuzi kupitia mtandao.