Maelfu ya bata watembea mamia ya kilomita

  • | BBC Swahili
    1,578 views
    Kila mwaka, maelfu ya bata hutembea kwa mamia ya kilomita kutoka Andhra Pradesh hadi Telangana baada ya mavuno ya mpunga kusini mwa India. Bata hao hula mbegu za mpunga zilizosalia, wadudu na magugu mashambani baada ya mpunga kuvunwa. Desturi hii ya miongo mingi hunufaisha pande zote mbili: wafugaji wa bata hupata kipato kwa kuuza mayai wakati wa kukaa kwao na wakulima wa mpunga hufurahia kinyesi cha bata kinachochangia kurutubisha udongo kwa njia ya asili, hivyo kuendeleza kilimo rafiki kwa mazingira. #bbcswahili #india #kilimo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw