Maelfu ya vijana wa Gen-z kutoka kaunti za Mombasa, Machakos, Makueni na Kisii kujitokeza

  • | Citizen TV
    4,946 views

    Maelfu ya vijana wa Gen-z kutoka kaunti za Mombasa, Machakos, Makueni na Kisii walijitokeza kusimama na familia za walioaga mwaka jana. Vijana hao waliteka barabara kuu mjini Mombasa huku polisi wakiandamana nao kabla ya kundi lililokodiwa kuharibu maandamano ya amani. Katika kaunti ya Makueni biashara katika mji wa wote zilisitishwa huku vijana wakiwasha moto katikati mwa barabara.