Maelfu ya wakazi wa Budalangi huko Busia wahangaika kutokana na mafuriko

  • | Citizen TV
    146 views

    Viongozi wa serikli katika eneo bunge la Budalangi kaunti ya busia wametakiwa kuwa macho ili kuhakikisha chakula cha msaada kwa waathiriwa wa mafuriko kilichoko katika ghala la makao makuu ya kaunti ndogo ya Bunyala, hakiuzwi. Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Bunyala Paul Papa amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba chakula hicho huuzwa na hata kupotea kutoka kwenye ghala hilo huku maelfu ya waliokusudiwa kufaidika wakiendelea kutaabika na njaa.