- 10,375 viewsDuration: 10:14Maelfu ya Wakenya wamejipata kwenye vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Urusi, na kuwacha familia kadhaa hapa zikiomboleza vifo au hata kupotea kwa jamaa zao. Licha ya familia nyingi kudai majibu kutoka kwa serikali, wengi wamesalia bila majibu ya walipo jamaa zao huku serikali ikikiri mtandao mpana unaohusisha hata maafisa wa serikali na wale wa usalama.