Maficho ya majambazi yageuzwa mashamba ya mahindi Baringo

  • | Citizen TV
    638 views

    Milima ya Korkaron na bonde la Tandare huko Baringo Kusini, ilikuwa ngome na maficho ya majambazi na wezi wa mifugo walioshambulia na kuua watu kiholela. Maeneo ya Sinoni, Seretion, Embossos, Arabal, na Kasiela yalikuwa hayapikiti miaka miwili iliyopita, na wale waliokuwa na ujasiri wa kwenda huko walilazimika kuwa na ulinzi wa magari yenye vifaa vya kijeshi ambapo maisha yao yalikuwa hatarini daima.