Mafunzo kuhusu afya ya uzazi yatolewa mashinani ili kukabili kusambaa kwa HIV

  • | Citizen TV
    993 views

    Huku wadau wakiibua hisia mseto kuhusu mafunzo ya afya ya uzazi katika shule za msingi, wizara ya afya nchini iko mbioni kubuni mbinu mpya za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi haswa miongoni mwa vijana. Hii ni baada ya takwimu za punde zaidi kuonyesha kuwa vijana wa kati ya umri wa miaka 15 hadi 29 wameandikisha zaidi ya asilimia 52 ya maambukizi. Laura Otieno anaangazia zaidi kuhusu mipango kwenye taarifa ifuatayo