Mafunzo ya uanabaharia kujumuishwa

  • | KBC Video
    5 views

    Wizara ya elimu inakadiria kufanyia marekebisho mfumo wa elimu ya umilisi ili kujumuisha masomo kuhusu masuala ya baharini katika juhudi za kutwaa fursa za ajira zinazoibuka katika sekta ya uchumi wa baharini. Hatua hiyo inalenga kuziba mianya iliyoko katika mfumo huo wa elimu na kuuwianisha na mahitaji katika sekta ya baharini. Waziri wa elimu Julius Migos amesema ipo haja ya kuimarisha ushirikiano baina ya wadau ili kubuni mfumo wa elimu unaotilia maanani sekta zote za kiuchumi. Uchumi wa baharini hushirikisha sekta mbalimbali zikiwemo uvuvi, kilimo cha samaki, utalii wa pwani, uchukuzi wa baharini miongoni mwa nyingine.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive