Mafuriko ya ghafla yavamia njia za chini za ardhi New York

  • | BBC Swahili
    965 views
    Abiria wa treni ya chini ya ardhi katika Jiji la New York walikwama ndani ya mabehewa baada ya mvua kunyesha na kusababisha mafuriko hadi ndani ya mabehewa. Video zilionyesha abiria wakitafuta namna ya kutoka ndani ya treni huku maji yakimiminika ndani ya kituo. Video nyingine zilionyesha abiria wakiwa wamepiga magoti juu ya viti ili kuepuka maji yaliyokuwa yanaingia ndani ya treni. #bbcswahili #NewYork #mafuriko Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw