Skip to main content
Skip to main content

Mafuriko yazidi kuathiri Narok na Tana River, Murkomen awataka wakazi kuhama

  • | Citizen TV
    2,154 views
    Duration: 3:26
    Watu wawili wameaga dunia katika Kaunti ya Narok baada ya kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Huko Tana River, wakazi wa eneo la Bakuyu wameanza kuhamia kambi za muda kufuatia tahadhari ya mafuriko iliyotolewa na mashirika mbalimbali pamoja na serikali. Haya yanajiri huku mvua iliyoshuhudiwa katika maeneo ya juu ikisababisha mabwawa ya Seven Forks kuvunja kingo. Akiripoti Maryanne Nyambura, Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewataka Wakenya wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko na hatari ya maporomoko ya ardhi kuhama mara moja.