Mafuta ya petroli yatarajiwa kupanda kwa zaidi ya shilingi 11 kwa lita

  • | Citizen TV
    3,208 views

    Hazina ya kitaifa inasema kuwa wakenya wanapaswa kujiandaa kwa nyakati ngumu zaidi ikiwa nchi haitaboresha hadhi yake ya kiuchumi. Ushuru wa mafuta ya petroli unatarajiwa kuongeza gharama ya bidhaa kwa zaidi ya shilingi 11 miezi ijayo. Kulingana na waziri wa fedha profesa njuguna ndungu, kuongeza ushuru ili kupunguza utegemeaji wa mikopo ni mojawapo ya hatua ambazo nchi itatumia.