Magavana wa maeneo ya Bonde la Ufa waunga mkono operesheni dhidi ya silaha haramu

  • | Citizen TV
    205 views

    Magavana wanaohudhuria kongomano la amani kanda ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa, wametangaza kuunga mkono oparesheni ya kusaka silaha haramu katika maeneo yenye utovu wa usalama. Magavana hao wakijumuisha George Natembeya wa Trans Nzoia na mwenzake wa West Pokot Simon Kachapin, wanasema utovu wa usalama umeathiri pakubwa shughuli za ugatuzi, wakitaka suala hilo kushughulikiwa kikamilifu. Sasa wanaitaka Idara ya Usalama kuwachukulia hatua wanasiasa wanaotoa maneno ya chuki, mbali na kuendelea kutwaa silaha zinazomilikiwa kinyume na sheria. Kongamano hilo litakalokamilika hapo kesho linawaleta pamoja magavana kutoka kaunti nane ili kutafuta mwafaka wa amani.